DEVICE FINANCING FAQ’S
Ni huduma gani hii Simu kwa Mkopo?
Hii ni huduma inayo wawezesha wateja wa Vodacom kununua na kumiliki simu kwa mkopo. Mteja anatakiwa kulipa kiwango cha awali kwanza na mkopo huu ulipa kidogo kidogo kwa muda wa miezi 9.
Nani anastahili huduma hii?
Mteja kupata huduma hii anatakiwa kuwa
Naweza vipi kufahamu endapo nastahili kupata simu?
Ili kufahamu kama unastahili unapaswa kujisajili ktk huduma kisha utapata ujumbe endapo unastahili ama la.
Aina gani ya simu ipo kwenye ofa ya simu kwa mkopo?
Tecno Pop 6
Naihitaji kulipa kiasi gani kama awamu ya kwanza ya kulipia simu ya Tecno Pop 6?
Kiwanga cha chini mteja anaweza kulipa ni Tshs. 20,000 ila mteja anarusiwa kulipa zaidi ya hichi kiwango.
Kiasi gani natakiwa kulipa kwa siku na kwa muda gani?
Kiwango cha kulipa kila siku ni Tshs. 1,000 ila mteja anaweza kulipa zaidi ya hicho kiwango. Malipo haya ni ya muda wa siku 270 (miezi 9).
Nalipaje mkopo wangu kila siku?
Kufanya malipo
- Piga *123#
- chagua ‘Mkopo wa Simu’ alafu ‘Rejesha Mkopo’
- Chagua kulipa kiwango cha siku au kuweka kiasi cha juu
- Ingiza PIN ya MPESA.
Naweza kurudisha muamala endapo nitakosea kufanya malipo?
Hapana,huwezi kurudisha muamala,piga huduma kwa wateja kwa maelekezo zaidi.
Nini kitatokea endapo nitashindwa kulipa marejesho ya siku?
Mteja atakayeshindwa kulipa rejesho la siku atapokea SMS na aina nyingine ya ukumbusho kufanya marejesho.Endapo hutolipa hatua mbalimbali zitafanyika ili kufungia huduma katika kifaa chako cha wasiliano
Nitapata vifurushi vya data na vya muda wa maongezi vya bure nikilipa kwa siku na wiki?
HAPANA,utahitajika kununua vifurushi vya data na muda wa maongezi
Njia ipi ya malipo inayotumika kulipia simu?
Malipo yote yatafanyika kwa kupita M-PESA
Naweza kumnunulia mtu mwingine simu?
Kwa sasa haiwekani.Laini ya simu unayofanyia malipo ni lazima iwe ktk simu uliyokopa.
Naweza vipi kuangalia salio langu la mkopo?
- Bonyeza *150*00#
- Chagua ‘Mikopo na Akiba”’ kisha chagua ‘Devices’
- Chagua “Taarifa za mkopo”
Je simu ina waranti
Simu zina waranti ya kiwandani ya mwaka mmoja.Vigezo na Masharti kuzingatiwa
Nikipata tatizo niyawasilishe vipi?
Tafadhali fika duka la Vodacom lililo jirani yako au muuzaji mkubwa wa bidhaa za Vodacom,au piga simu huduma kwa wateja namba 100
Nini kitafanyika kama nitashindwa kufanya malipo na muda ukapita?
Utashindwa kufikia applications,meseji na huduma za kupiga simu zitaondolewa taratibu endapo hutolipa marejesho yako ndani ya muda.Simu yako ikifungwa utaweza kupiga simu kwa huduma kwa wateja na namba za dharula pekee.Ingia ktk menu ya MPesa *150# au ktk application ya malipo na ulipe ndani ya muda au rejesha kwa kutanguliza malipo kuepuka hayo.
Nifanye nini endapo Simu yangu itapotea ama kuibwa?
Toa taarifa ya wizi katika kituo cha polisi cha jirani yako.Tafadhali fahamu kuwa utahitajika kuendelea kufanya malipo kwa muda wote wa hadi malipo ya mwisho
Simu yangu ikiharibika nifanye nini?
Kama ni ndani ya muda wa mwaka mmoja wa marekebisho ya bure,taarifu huduma kwa wateja na fika kwa wakala maalum wa Tecno kwa ajili ya matengenezo
Was this article helpful?
That’s Great!
Thank you for your feedback
Sorry! We couldn't be helpful
Thank you for your feedback
Feedback sent
We appreciate your effort and will try to fix the article